[PR] Gain and Get More Likes and Followers on Instagram.

#kuperuzinakudadisi

630 posts

TOP POSTS

Lungu akataa biashara ya uswahiba bandari
|
RAIS wa Zambia, Edgar Lungu ameitahadharisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuwa Wazambia hawabanwi na urafiki uliopo kati ya nchi hizi mbili kupitisha mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam, bali wanaendelea kufanya hivyo kutegemeana na ufanisi unaofanywa na mamlaka hiyo.

Akizungumza baada ya kutembelea baadhi ya vitengo vya bandari hiyo jana, Rais Lungu alisisitiza nchi yake itaendelea kupitisha mizigo kwenye bandari hiyo kama itaendelea kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa kuliko bandari zingine zilizoko katika ukanda wa kusini mwa Afrika. “Mimi na Rais Magufuli (John) tuna urafiki wa karibu, nchi mbili hizi pia zina urafiki wa muda mrefu, lakini Wazambia hawapitishi mizigo yao katika bandari hii kwa sababu ya urafiki wetu, bali wanachohitaji ni urahisi na uharaka wa kutoa na kusafirisha mizigo yao. “Pia hatuwaungi mkono kibiashara eti kwa sababu tu nchi mbili hizi tuna uhusiano mzuri, bali tunaangalia ni wapi ambako wanatoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi...kwani naamini hata tusipowapa biashara undugu wetu wa damu utaendelea, lakini hatuendi kwingine tunakuja hapa kwa sababu ya ufanisi,” alisema Rais Lungu.

Rais huyo pia aliitahadharisha mamlaka hiyo kuwa wanatakiwa kuhakikisha kila siku wanabuni namna ya kuboresha huduma zao kwa kuwa kuna nchi jirani pia zinatoa huduma kama wanayotoa wao na ambao wangependa kupata biashara zaidi. #KuperuziNaKudadisi #HabariLeo

SMZ yampiga 'stop' Maalim Seif kutumia misikiti.
|
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibada kwa shughuli za kisiasa Visiwani Zanzibar.

Msimamo huo wa Serikali umekuja siku chache tangu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kutumia kila siku za Ijumaa kufikisha ujumbe katika msikiti atakaoswali.

Akitoa tamko la Serikali jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa yote ya Zanzibar kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika mikoa yao. “Kwa taarifa hii Serikali inawaagiza wakuu wa mikoa kupitia kamati zao za ulinzi na usalama kusimamia utekelezaji wa agizo hili katika mikoa yao,” alisema Waziri Aboud.

Alisema Serikali imewaagiza wakuu hao wa mikoa kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo. #KuperuziNaKudadisi #Mtanzania

Ufaulu juu Darasa la 7 wavulana watamba
|
UFAULU kwa watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.

Aidha, watahiniwa 238 kutoka shule sita wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani huo.

Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.

Kati ya wanafunzi hao 10, watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani Shinyanga, wawili Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera. Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250. “Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwapo ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” alisema Dk Msonde.

Watahiniwa 16,929 wamepata daraja A, watahiniwa 141,616 wamepata Daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E . Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06 na 14.76 ikilinganishwa na mwaka 2015 huku masomo ya Kiswahili, Hisabati na Kiingereza ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 0.39 na 12.51 ukilinganisha na mwaka jana.
#KuperuziNaKudadisi
#HabariLeo

Biashara ya Bangi tishio nchini.
|

Dar es Salaam. Japokuwa Jeshi la Polisi limejitahidi kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, ripoti ya Hali ya Dawa za Kulevya ya 2015 imeeleza bangi ndiyo inayoongoza Tanzania.

Juzi, jeshi hilo lilikamata viroba 251 vya bangi mkoani Pwani. Pia, katika msako uliofanyika mkoani humo zilibaini ekari tatu za shamba la bangi lililokuwa linaendesha kilimo cha umwagiliaji na yalikamatwa magunia 32 ya mbegu za zao hilo haramu.

Kwa mwaka jana, ekari 50 za mashamba ya bangi ziligundulika na kuteketezwa na Polisi. #KuperuziNaKudadisi #Mwananchi

Walimu, Polisi, walemavu mwisho kusafiri bure mwendokasi.
|
LICHA ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika utoaji huduma wa magari yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (DART), Kampuni inayoendesha mradi huo, UDART imepiga marufuku usafiri wa bure kwa makundi mbalimbali wakiwemo askari polisi, walemavu, viongozi wa dini na hata walimu.

Imesema mageti yaliyokuwa wakiyatumia yafungwe na kila mmoja alipe. Udart imetoa taarifa hiyo katika waraka uliobandikwa katika kila kituo mwishoni mwa wiki na kufafanua kuwa kumekuwepo na ongezeko la makundi hayo, wakipita katika mageti hayo bila kulipa na pia kupokea simu kutoka katika makundi mbalimbali, yakiomba kupatiwa huduma hiyo.

Hilo limo katika waraka uliosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa na nakala kwenda kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Msajili wa Hazina na kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra). Katika taarifa hiyo, Mgassa alitaka waraka huo ufike kwa watumishi wote wa usafiri huo na hatua zichukuliwe haraka. Alisema watumishi waliopo katika vituo wanapaswa kuhakikisha mageti yanakuwa yamefungwa kwa ufunguo na hakuna anayeruhusiwa kupita bila kulipa.

Makundi hayo yalikuwa yakisafiri bila kulipa nauli katika mradi huo unaofanya kazi katika Barabara ya Morogoro na ile ya Morocco jijini Dar es Salaam. #KuperuziNaKudadisi #PowerBreakFast #HabariLeo

Serikali kutumia trilioni 32.9/- mwaka 2017/2018
|
SERIKALI imepanga kutumia Sh trilioni 32.946 katika bajeti yake ya mwaka 2017/2018, ikiwa imeongezeka kutoka Sh trilioni 29.5 ya mwaka 2016/2017 na kutaja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuzingatia miradi ya kufufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha na kuendeleza maeneo ya viwanda vidogo.

Sambamba na hilo, serikali imebainisha mikakati yake ya kudhibiti matumizi, ambapo sasa itahakikisha mikataba inayoingiwa na serikali na taasisi zake inakuwa katika shilingi za Tanzania, isipokuwa kwa mikataba inayohusisha biashara za kimataifa.

Kuhusu kuhamishia shughuli za makao makuu ya serikali Dodoma, mipango ya ujenzi wa majengo na miundombinu yote ya serikali iliyopangwa kujengwa Dar es Salaam, itahamishiwa Dodoma.

Akiwasilisha bungeni jana mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/2018, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kati ya Sh trilioni 32.946, Sh trilioni 19.782 zitatengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. “Sh trilioni 7.206 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa serikali na taasisi za umma na Sh trilioni 9.723 ni kwa ajili ya kulipia deni la Taifa lililoiva. Matumizi ya maendeleo yatakuwa Sh trilioni 13.164 sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ambapo fedha za ndani ni Sh 9.960 sawa na asilimia 76. Kiwango hiki ni ongezeko la Sh trilioni 1.343 ikilinganishwa na mwaka 2016/2017,” alifafanua.

Alisema mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh trilioni 20.872 sawa na asilimia 63 ya mahitaji yote.

Kati ya mapato hayo serikali inatarajia kukusanya mapato ya kodi ya Sh trilioni 18.097 sawa na asilimia 87 ya mapato ya ndani.
#KuperuziNaKudadisi
#HabariLeo

JPM awatumbua waliomdanganya uwanja wa ndege
|
RAIS John Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam upande wa Terminal One na kuagiza maofisa wawili, waliotoa taarifa za uongo kwake Mei mwaka huu, wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Mei mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja huo akitokea jijini Kampala nchini Uganda, ambako alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni. Alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

Lakini jana baada ya kumsindikiza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alikuwa akiondoka nchini baada ya ziara ya siku tatu, aliamua kufanya tena ukaguzi wa kushitukiza, na mara hii amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.

Hata hivyo, amemuagiza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wawili waliotoa taarifa za uongo alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza. “Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona, lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua,” alisisitiza Dk Magufuli, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana.

Rais Magufuli aliagiza maofisa hao, ambao kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, ni Lilian Minja na Novia Maduka ambao ni maofisa oparesheni wa JNIA, washushwe vyeo. #KuperuziNaKudadisi #HabariLeo

Kabila: Natamani DRC iwe na Amani kama Tanzania🇹🇿
|
RAIS wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila amebainisha wazi kuwa anatamani nchi yake pamoja na ukubwa na utajiri iliyonayo, ingekuwa na amani na mshikamano kama Tanzania.

Pia Rais huyo amesisitiza kuwa nchi yake kwa sasa iko tayari kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi nyingine ikiwemo Tanzania, tofauti na zamani ambako ilijikita zaidi katika masuala ya kutafuta amani. Kabila aliyasema hayo juzi usiku wakati akizungumza kwenye dhifa ya chakula aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alisema anavutiwa na hali halisi ya amani inayoendelea kudumu nchini Tanzania, ikiwemo jitihada za wananchi na serikali kwa ujumla katika kuitunza na kuilinda amani hiyo na kuimarisha uchumi. “Kila nikipita katika mitaa mbalimbali ya DRC nakumbuka hali halisi ya amani iliyopo Tanzania. Nikiri tu nimekuwa nikivutiwa sana na hali ya amani na mshikamano iliyopo hapa Tanzania. DRC ni nchi kubwa na yenye utajiri, ninaiombea sana nchi yangu na yenyewe ifurahie amani hii,” alisisitiza. #KuperuziNaKudadisi #HabariLeo

Shein asaini muswada wa mafuta, gesi
|
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesaini muswada wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ambao sasa utaipa ruhusa Zanzibar kisheria kutafuta nishati hiyo kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.

Utiaji saini huo ulifanyika Ikulu na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Dk Shein alisema rasilimali ya mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa kwenye orodha ya Muungano ambayo usimamizi wake kabla ya kutungwa kwa Sheria Namba 21 ya 2015 ilikuwa chini ya Shirika la Maendeleo la Mafuta (TPDC) pamoja na Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta, Sura ya 328, sheria ambayo ilikuwa inatumika pande zote mbili za Muungano.

Hata hivyo, alisema mfumo huo uliokuwepo ulionekana kuwa na upungufu na kubwa zaidi mfumo huo ulikuwa hautoi fursa kwa SMZ na watu wake katika kusimamia rasilimali ya mafuta na gesi asilia. Pia, haukutoa fursa kwa Zanzibar katika muundo wa kiutawala wa taasisi zinazosimamia utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Alisema kwa sababu suala la mafuta ni uchumi, SMZ ilipendekeza kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa suala la mafuta na gesi asilia liachiwe kila upande wa Muungano kusimamia rasilimali hiyo pamoja na mapato yake.

Hata hivyo, suala la mafuta na gesi asilia halijaondoka kwenye Katiba ya Muungano, Sheria ya Bunge imetambua hilo na imeweka usimamizi wa rasilimali hiyo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kusainiwa kwa sheria hiyo sasa inafungua milango kwa kampuni na taasisi mbalimbali zenye nia ya kuchimba mafuta na gesi asilia kwenda Zanzibar kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
#KuperuziNaKudadisi #HabariLeo

MOST RECENT

#kuperuzinakudadisi. . GazetilaMtanzania
na Alichokisema IGP Sirro kuhusu kumtangazia Kiama #MangeKimambi.

Most Popular Instagram Hashtags