[PR] Gain and Get More Likes and Followers on Instagram.

#fikicha

98 posts

TOP POSTS

"Ukweli usiotuhusu ukiuleta kwetu ni kutuonea tu, bora unyamaze. Kuwa makini na unaongea nini na unaongea na nani hata kama unachoongea sio uongo"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Mara nyingi Mungu hutupa watu kabla ya kutufikisha kwenye kusudi alilotuumbia kulifikia, unavyoshindwa kuwatumia ndivyo unavyojichelewesha kufika kwenye kilele cha mafanikio yako." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Unapoongea vitu vigumu kwa lugha nyepesi haifanyi vitu hivyo Kuwa vyepesi bali unawafanya wanaokusikiliza kuamini uwezo wao ni mkubwa kuliko vitu hivyo na hiyo ndio maana ya kuhamasisha." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Nimesikia watu wanapenda kusema 'nakupenda bure' au 'Nisamehe bure'. Hivi hamjui kupenda ni gharama; vipi kwenu kuna watu wanasamehe kwa pesa?" #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Unapokuwa kijana hizi hatua 4 ni za muhimu sana sana, sababu chaguzi hupungua kwa kadri umri unavyosonga CHAGUZI ⬇ TAFAKARI ⬇ MAAMUZI ⬇ MATOKEO

Matokeo yeyote ni matokeo ya chaguzi tulizofanyia maamuzi iwe kwa kutafakari au kutokutafakari"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

FUTA

Baada ya kuliona, kosa ulilolifanya,
Hakuna tena namna, wala usije danganya,
Na usiseme hapana, kwamba wewe hajafanya,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.

Hatufuti kwa kubisha, Kumbe kosa umetenda,
Utakuwa wajichosha, Wajiwekea kidonda,
Moyo wajihuzunisha, Wajua ulivyotenda,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Huna furaha moyoni, makosa ndio sababu,
Kosa hutafuna ndani, ukikataa kutubu,
Huiondoa amani, dhamiri yakusulubu,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Unapotubu tambua, usilete mazoea,
Nikikosa namwambia, Mi mwanadamu ajua,
Hayo makosa jutia, amua hutarudia,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.

We si wakwanza kukosa, kwamba watu watacheka,
Nisamehe nimekosa, waungwana hutamka,
Ujifunze kwao sasa, kwenye kosa utatoka,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Msamaha una nguvu, kuyaponya majeraha,
Unakupa utulivu, pia moyo wa furaha,
Watu wale wapumbavu, hukimbia msamaha,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Ukiombwa usamehe, sio hadi usifiwe,
Msamaha Si sherehe, na zawadi uletewe,
Kazi yako ni samehe, na kinyongo uondowe,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea. Kweli amekukosea, Sikatai natambua,
Unapo mfikiria, hasira kumjengea,
Maumivu wapalia, bora tu kumuachia,
Kwa kupenda kusamehe, Maumivu unafuta.
Kovu laweza bakia, lisije kushikiria,
Ushindwe kumuachia, samehe na achilia,
Wewe unayopitia, wengine washapitia,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea.
Siwezi kulazimisha, hatua wewe chukua,
Mimi nimeelimisha, ni wewe wakuamua,
Jambo lako linatisha, ila ni ishatokea,
Kuacha au kufuta, wewe ndie changanua.
#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya +255 717 567 500
somavitabuleo@gmail.com

SIJUI UPO KUNDI LIPI A. B.
Safi vs Nadhifu
Uzuri vs Ubora
Kujali. vs kupenda
Elimu. vs maarifa
Hodari vs Shujaa
Maarufu vs Mashuhuri
Wengi wetu tunayapenda mambo ya kundi la kwanza na inawezekana tunayo kwa asilimia zote. Na mara nyingi mambo hayo hutupa kiburi au hututengenezea mazingira ya kujivuna

Ni wachache hupenda mambo ya kundi la pili. Wengi huyapenda kwa mdomo lakini hawana kwa vitendo. Kwa sababu yanahitaji nidhamu ya ziada kuyapata.

Tofauti kubwa kati ya mambo hayo ni kwamba unaweza kuwa na mambo ya kundi la kwanza lakini usiwe na ya kundi la pili lakini huwezi kuwa na ya kundi la pili usiwe na ya kundi la kwanza. Mfn unaweza kuwa na elimu ila usiwe na maarifa au ukawa hodari lakini usiwe shujaa

Kumbuka:
Unaweza ona kama viko sawa lakini haviko sawa. Tofauti yake ni kubwa kuliko nyeupe na nyeusi

#Fikicha Akili#

Kila kitu kinatengenezwa
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

KONDAKTA NA ABIRIA

Abiria : Hivi nyie makodakta mtaanza lini ustaarabu 'aliongea kwa ukali'

Kondakta : Tumeanza leo na sasa hivi.

Abiria : Mbona nimekuomba msaada unishushe hapo umegoma?

Kondakta : Konda mstaarabu humshusha abiria kwenye kituo halisi kinachotambulika.
Abiria : Mbona mnapakia popote pale kwenye kushusha ndio mnaleta ujuaji.

Kondakta : Unaweza pokea pesa kwa mtu yeyote lakini hupaswi kutoa pesa kwa yeyote. Maana unapopokea unaweza amua kuzirudisha kwa kuwa zipo mikononi mwako ila ukitoa unaweza usirudishiwe. Na huo ni ustaarabu unaweza jifunza kwetu makonda.

Abiria : Kwa hiyo unajitia mjuaji?

Kondakta : Kwasababu wewe hujui lolote ndio maana unataka kama ulivyopanda popote ndivyo ushushwe popote.
Abiria : Si nimekuomba lakini.

Kondakta : Ndio maana mnaonaga Mungu hawajibu mkimuomba. Mungu anakujibu ukiwa kwenye kituo, ila anakuchukua ukiwa Katika hali yeyote mbaya hana hiana anakuchukua harafu anakufundisha utaratibu.

Abiria : Kwa hiyo unamuingiza Mungu kwenye uonevu wako. Unadhani anakusikiliza

Kondakta : Basi muingize wewe kwenye uonevu ulioonewa.
Dereva : Kwani tatizo nini 'dereva aliingilia huku akicheka'

Abiria : alichonifanyia konda wako unadhani ni kitu kizuri.

Kondakta : Sio huyo mwalimu wa ustaarabu wakati yeye mwenyewe sio mstaarabu. Amekaa siti ya mbele baada ya kukuomba wewe dereva umshushe anahangaika na konda sio mstaarabu.

Dereva : Mimi nimemnyamazia anaongea ustaarabu wakati amepanda kwenye gari tuko wawili tu huku hata salamu hajatoa. Halafu... Abiria wengine : Kicheko hahahahaha
Kondakta : Haya mstaarabu shuka hiki ndio kituo
Abiria : Tutakutana tu jifanye mjanja.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

KUTOA KUBAKIZA MOJA

Unapofanya maamuzi unakuwa na chaguzi nyingi. Unazipunguza zinabaki chache, na katika chache kuna moja linakuvutia na linaonekana na nguvu kwako na unaamua kulichukua kwa kuamua. Unakuwa umetoa yote na umebakiwa na moja.

Ulipohamia huo mji ulikuta makanisa mengi sana. Na yote ni mazuri, lakini katika yote ukaamua kuchagua moja na kuwa kanisa lako unalotambulika Kuwa u mshirika. Hapo napo umetoa mengi umebakia na moja.

Kabla hujaoa/hujaolewa ulifuatwa au uliona wengi sana. Wazuri wa kila rangi, wenye maumbo na mwonekano wa kila namna. Lakini uliamua kuwatoa wote na kubakia na mmoja. Hiyo pia ni kutoa kubaki na moja.

Kuna Mungu na Ibilisi, kwenda nao wote haiwezekani inabidi tu utoe ubaki na mmoja. Hiyo nayo ni kutoa na kubaki na moja.

Nimekuja kugundua katika maisha watu wanapenda kubaki na vingi. Yaani watoe vichache wabaki na vingi. Sasa katika mambo muhimu karibia yote unalazimika kubaki na moja. Sasa wengi hatupendi ndio maana
-Tuna watu wasio na msimamo wao ni ndumilakuwili mtu wa nia mbili.
-Tuna watu hawajulikani wanaabudu wapi. Wao ni kama watalii kila mbuga twende tu.
-Tuna watu hawana maono wao kila njia twende. Kila mtu maarufu au aliyefanikiwa anataka kuongozana naye.
-Tuna watu wao hawataki kuoa sio kwamba hawezi kupata mwanamke mmoja hapana ila anataka abaki hivyo ili kila anayemtaka awe naye.

Hayo na mengine mengi yanahitaji mtu anayeamua kutoa na kubaki na moja.
Uzuri ni kwamba ukifanya maamuzi mazuri ya katika mambo ya kubaki na moja. Basi hiyo moja itakusaidia kukupa vitu ambavyo ulivyoondoa visingeweza kukupa. Chagua kubaki na moja ambayo ndani yake hiyo moja kuna vingi furaha na amani na utajiri vikiwemo kati ya vingi vinavyopatikana ndani ya hiyo moja.

Ufunguo.
KUTOA=KUONDOA.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

MOST RECENT

Happy born day mai πŸ‡§ πŸ‡· πŸ‡΄ πŸ‡Ή πŸ‡­ πŸ‡ͺ πŸ‡· live long life unapoongeza mwaka mwingine πŸ‡² πŸ‡Ί πŸ‡³ πŸ‡¬ πŸ‡Ί akupe kibali....... Mwalimu wetu Mungu akupe maarifa mengi,
#to be is to do
#fikicha akili
#watengeneze kizazi
#pendo penzini

"Ukikataliwa haimaanishi ndio huwezi fanikiwa, ukitengwa haimaanishi ndio mwisho wa ndoto zako. Ila ndio mwanzo wa kupata watu watakaoshuhudia mafanikio yako wakiwa mbali, songa mbele"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Walinikaririsha badala ya kunielewesha cha ajabu wakakumezesha bila kukutafakarisha. Sasa nimeshituka ninaanza kuhoji unaniona sina nidhamu na unaniita mjuaji huku unasahau hata kusema hivyo ni umekaririshwa." #Fikicha Akili#

JIULIZE KWA UPOLE
Mwl Makwaya
Kuwa ni Kufanya.

"Kiwango cha heshima hakiwi kikubwa kwasababu una umri mkubwa, bali kinaongezeka kwa vile unavyowatendea wengine na kwa namna unavyovaa na kuongea mbele za watu bila kusahau tabia yako." #Fikicha Akili#

"Kabla hujagoma au kukubali tafadhari lazima ujue kuna maisha baada ya tukio. Ukilijua hilo hutakubali kubali tu au hutagoma goma tu tofauti na hivyo utaishia kulalamika hakuna anayetaka kufanya kazi na wewe." #Mahusiano yana nguvu kuliko tukio#

Salamu kwa wenye vipaji onekana

#Fikicha Akili#

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

UJUMBE WA LEO

#Repost @mwlmakwaya
・・・
"Ufahamu-Huona picha
Nia-Hutafuta njia
Akili-Hutengeneza namna
Maarifa-Huonyesha mipaka
Hekima-Huongoza maamuzi"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kiwango cha heshima hakiwi kikubwa kwasababu una umri mkubwa, bali kinaongezeka kwa vile unavyowatendea wengine na kwa namna unavyovaa na kuongea mbele za watu bila kusahau tabia yako." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Moja ya shule ngumu wengi hufeli, ni kipindi unadharauliwa wakati unajua na ni kweli ulistahili heshima. Ukiwa kwenye kipindi hiko tafadhari kuwa makini na mawazo pamoja na maneno yako." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ukiwa kazini fanya kazi usiogope watu watakuchukuliaje cha muhimu iwe kazi halali, na hivyo ndivyo walivyo wapiga picha wengi wanachojali ni picha itokee vizuri wala hawaangaiki na watu watawaonaje namna wanavyoipiga hiyo picha"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Mungu hawezi kukupa muonekano mzuri (umbo) ili huo muonekano ukuharibu, mtu hujiharibu yeye mwenyewe kwa kutokujua kwanini anamuonekano huo alionao "

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kuwekeza pesa, muda, akili na nguvu nyingi katika jambo moja huleta matokeo yatakayorahisisha kuyapata yale ambayo hukuwekeza sana vitu hivyo vinne, na hiyo ndio hekima iliyowashinda watu wengi waliovigundua vipaji vyao mapema"

Patia kisha wekeza

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ufahamu-Huona picha
Nia-Hutafuta njia
Akili-Hutengeneza namna
Maarifa-Huonyesha mipaka
Hekima-Huongoza maamuzi"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kupendwa ni hitaji muhimu sana lakini kupenda ni hitaji muhimu zaidi. Na Kwasababu kupenda kunapotea duniani na kunakimbilia katika sayari ya pesa na mali, ukifundisha kila mtu kupenda basi kila mtu atapendwa"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kuanza upya baada ya kuanza hakujawahi kumkatalia muanzaji kuanza, maana haipingiki Kuwa; kuna mianzo mingi katika mwanzo mmoja cha muhimu ufike mwisho wa mwanzo kusudiwa"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Unaweza kuwa na nguvu ya kuwashinda wanaume kumi kwa mabavu na hata kwa hoja, lakini wakiamua kutumia mwanamke mmoja mlaghai wanaweza kukushinda bila wao kuwepo endapo tu utajidanganya nguvu za kuwashinda wanaume kumi ndizo utatumia kumshinda mwanamke laghai mmoja. Kama unabisha muulize Samsoni"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ni rahisi kuwashinda watu elfu moja kwa hoja zenye nguvu lakini sio rahisi kushinda sifa unazopewa na watu kumi wa karibu, haswa kama hawajui kukukosoa. mashujaa wengi walishindwa na mtu mmoja tu aliyejua kusifia kinafiki"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Mwalimu mbona unapenda kusoma vitabu vya zamani?
Mwl: Kwanini vya sasa sivisomi?
Sijasema vya sasa huvisomi ila nakuona sana na vitabu vya zamani.
Mwl: Napenda hekima za wazee walipokuwa vijana"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Ukidanganywa kwa maneno ya ushawishi utabadilisha na maana halisi ya maneno halisi"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

MIMI NA YEYE

Mtu mmoja alinifuata na kuanza kuongea na mimi kuhusu huduma haswa kwa vijana.

Yeye : Mwalimu napenda sana unavyofundisha na kushauri.

Mimi : Asante sana.
Yeye : Natamani kweli Kuwa mwalimu wa vijana.

Mimi : Unatamani kuwa unafundisha nini na nini kwa hao vijana.

Yeye : Natamani sana sana mahusiano na kujitambua.

Mimi : Ushajua ni nini na nini unahitaji kuwa navyo ili uweze kufundisha.

Yeye : Nadhani natakiwa kuwajua vijana wanataka nini, niwe rafiki yao. Lakini pia nisome sana vitabu kuhusu vijana na kujua jinsi ya kujichanganya nao.

Mimi : Kati ya hivyo unafikiri umepungukiwa kipi?
Yeye : sijajua namna ya kuanza maana sina connections kama ninyi, ndio maana nimekufuata.

Mimi : Kuna kitu unatakiwa kuwa nacho kabla ya hivyo vyote. Na ukikikosa hiko hufai Kuwa karibu na vijana.

Yeye : Ni kitu gani hicho?
Mimi : Kamuombe Mungu akupe moyo wa Telabite(GB 1000) kwa kuanzia sio mbaya.

Yeye : "Huku akiwa ameshituka maana hakutegemea jibu hilo"
Kwanini moyo wa Telabite.

Mimi : Kwasababu ukiwa na moyo wa kb, mb au gb Kwa mambo ya vijana utapasuka na utaishia Kuwa sadukayo au falisayo kwa hao vijana.
Yeye : Basi ngoja nikatafakari tena.

Mimi : Ukitaka kutafakari vizuri nenda kwenye mkesha wa vijana ukae nyuma halafu kimya. Ukitoka hapo nenda chuoni week end jumamosi alfajiri kakae getini kuanzia saa 10 alfajiri. Kisha uje unifuate nitajua kama una moyo wa TB.
Yeye : Kazi yote hiyo ya nini

Mimi : Basi kazi hii haikufai. Katumike kwenye eneo lingine.

Yeye : mbona mwalimu unanikatisha tamaa?

Mimi : Nikukatisha wewe liunge.
#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Usiishi kwa mategemeo ukasema ni imani, mategemeo ni pata potea wakati imani ni hakika"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ukweli usiotuhusu ukiuleta kwetu ni kutuonea tu, bora unyamaze. Kuwa makini na unaongea nini na unaongea na nani hata kama unachoongea sio uongo"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ukweli usiotuhusu ukiuleta kwetu ni kutuonea tu, bora unyamaze. Kuwa makini na unaongea nini na unaongea na nani hata kama unachoongea sio uongo"

#Fikicha Akili#

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

Kunawiri vs Kupendeza
Uzuri vs Urembo
Kufahamu vs Kujua
Kutafakari vs Kuwaza

Toka nje ya jengo ila sio darasani.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Jinsi ambavyo unajifunza na kujua sana, ndivyo unagundua hujui mengi. Na jambo hilo linatosha kukomesha dalili yeyote ya dharau ndani yako"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Karibia watu wote unaowasikia wamefanya mambo makubwa walikuwa na hii sifa kubwa moja inayofanana. KUJUA NANI AKAE WAPI NA AFANYE NINI." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni kufanya

"Kisha nikaona janga chini ya jua kwamba wale walioigharamia elimu wengi wao wameiokosa angalau walibaki na karatasi na wakavaa gauni; na wale waliogharamia kutatua changamoto wengi wao wakaipata elimu na kubaki kuwatumikisha wale waliogharamia elimu na kuikosa. Hii ni ajabu na kushangaza sana"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

#Repost @mwlmakwaya (@get_repost)
・・・
"Ukipenda kusifiwa usichukie kukosolewa na ukivuka hapo tunakuita muelewa, ukipenda kukosoa jua na kusifia usipovuka hapo tunakuita mjuaji "

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kuwasema vibaya waliofanikiwa hakukuongezei elimu ya wewe kufanikiwa. Ila wewe kufanikiwa kunakupa kuona maeneo mengi ambayo hujafanikiwa, Na moja ya maeneo unatakiwa kufanikiwa ni kuwafanya wengine kufanikiwa." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ukiona kila ukimuona tajiri unaanza kuwaza uchawi, rushwa, freemasons; ujue tu, wewe ni zaidi ya mtu mwenye pepo wa utambuzi. Maana wenye pepo la utambuzi hawawezi kuwa matajiri bali hutajirisha wengine"

#Fikicha Akili#

Ukweli Mgumu Mtamu

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Uchawi sio lazima ubebe tunguri; hata kukasirika kwasababu mwenzako amefanikiwa ni uchawi pia." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kila mtu alijikuta amezaliwa. Kujikuta unafanya mengine bila kujua kwanini unafanya, hiyo siyo kujikuta bali umejipeleka kwa kujua au kwa kutokuwa makini. Tafadhari usipende kujikuta"
#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Usipokuwa makini katika kusikiliza ushauri unaweza jikuta unapotezwa na washauri haswa kama hao washauri hawajui wapi unapokwenda. Ni kweli tunahitaji washauri lakini washauri wanaokutoa kwenye njia ya kusudi la Mungu ndani yako hao ni wauaji"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Ukipenda kusifiwa usichukie kukosolewa na ukivuka hapo tunakuita muelewa, ukipenda kukosoa jua na kusifia usipovuka hapo tunakuita mjuaji "

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Ukiona unataka/unang'ang'ania kipaji kithaminiwe na wengine kwa nguvu, ujue tu wewe hujakithamini maana siku ukikithamini sawasawa wa nje wataitikia uthaminishaji wako. Watu wanashindwa kukithamini maana unachofanya ni kama kuimbisha pambio kwa sauti ya kuitikia kisha unataka watu wafurahie pambio yako"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Maneno Kiburi na kibuti yametofautiana kwa herufi moja tu, hiyo tofauti imeletea maana mbili tofauti. Ila kuna jambo moja yamefanana, husumbua moyo wa mpumbavu kwa muda mrefu"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Unapoongeza kasi ya Kufanya jambo lolote kumbuka kuongeza umakini mara mbili ya kasi yako, tofauti na hapo ni rahisi hiyo kasi kukuua"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Kutumia nguvu bila akili inaweza kuwa sawa na kutumia elimu bila hekima, usitutishe na nguvu wala elimu yako kama huna akili na hekima basi nguvu au elimu yako vinaweza tumika kukuangamiza wewe mwenyewe"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Kuna watu wanalisha sana tumbo kuliko kichwa, wanapenda kula kuliko kusoma, kujifunza, wala kufikiri. Ukiona hujawahi fanya kazi na ukasahau kula basi ujue tumbo lishakuponza au liko njiani kukuponza kuendelea kufanya kazi/jambo usilolipenda ila unafanya ili ule tu." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

KUNA WAKATI
Unatamani kulala huna usingizi
Unatamani kulia huna machozi
Unatamani kula lakini huwezi
Kuna wakati katikati ya nyakati.
Umefanya jambo ila hulifurahii
Muda uende lakini hausogei
Unajituma kumbe huna bidii
Kuna wakati katikati ya nyakati.

Unaona mambo hayaendi
Yanakutokea mambo huyapendi
Unaona hutakuwa mshindi
Kuna wakati katikati ya nyakati.

Unapambana na uvivu
Unashindana na uchovu
Unahangaishwa na wivu
Kuna wakati katikati ya nyakati.
Wengine wakufurahia
Wewe wajishangaa
Huoni ukipiga hatua
Kuna wakati katikati ya nyakati.

Mambo Yanakutokea
Yale usiyo tarajia
Unawaza na kuwazua
Kuna wakati katikati ya nyakati.
Unaweza kukurupuka
Waweza jikuta walopoka
Kama sio kufokafoka
Kuna wakati katikati ya nyakati.

Ukiwa kwenye hizo nyakati
Tulia tafakari huo wakati
Usije mwenyewe ukajisaliti
Kuna wakati katikati ya nyakati.
Tungo tungoni
#Fikicha Akili#

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

"Kama hujawahi kupigwa kibuti kuna utamu wa kupenda hujawahi kuuonja, sio kwamba nataka upigwe kibuti, hasha! Ninachokufundisha ni kwamba kufeli nalo ni darasa, wengi hupitia halafu wanafeli, wanaofaulu katika kufeli huelewa zaidi utamu wa kufaulu." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

Mwalimu Makwaya Styled and Dressed by JonesFAD.
Karibu.

#Rensta #Repost: @mwlmakwaya via @renstapp Β·Β·Β·
β€œ SIJUI UPO KUNDI LIPI A. B.
Safi vs Nadhifu
Uzuri vs Ubora
Kujali. vs kupenda
Elimu. vs maarifa
Hodari vs Shujaa
Maarufu vs Mashuhuri
Wengi wetu tunayapenda mambo ya kundi la kwanza na inawezekana tunayo kwa asilimia zote. Na mara nyingi mambo hayo hutupa kiburi au hututengenezea mazingira ya kujivuna

Ni wachache hupenda mambo ya kundi la pili. Wengi huyapenda kwa mdomo lakini hawana kwa vitendo. Kwa sababu yanahitaji nidhamu ya ziada kuyapata.

Tofauti kubwa kati ya mambo hayo ni kwamba unaweza kuwa na mambo ya kundi la kwanza lakini usiwe na ya kundi la pili lakini huwezi kuwa na ya kundi la pili usiwe na ya kundi la kwanza. Mfn unaweza kuwa na elimu ila usiwe na maarifa au ukawa hodari lakini usiwe shujaa

Kumbuka:
Unaweza ona kama viko sawa lakini haviko sawa. Tofauti yake ni kubwa kuliko nyeupe na nyeusi

#Fikicha Akili#

Kila kitu kinatengenezwa
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya. ”

DHANA

Tangu kipindi cha utotoni
Kabla hata ya kwenda shuleni
Tukawekewa dhana akilini
Mkubwa kamwe hakosei
Tukapelekwa shuleni
Tukaingia darasani
Tukajazwa tena akilini
Kwamba mwalimu ajua yote.
Tulipofika la nne
Tukaongezewa lingine
Likawashinda wengine
Eti kujua Kiingereza umeelimika

Tulipotoka shuleni
Likachipua laulimbukeni
Ukisoma hukai kijijini
Tena lazima uajiliwe serikalini

Tulipojichanganya ulimwenguni,
Ndio tukamezeshwa moyoni
Wengi hapo wamejikataa ndani
Mzungu hawezi Kuwa masikini

#Fikicha Akili#

Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya

#Repost @mwlmakwaya
・・・
FUTA

Baada ya kuliona, kosa ulilolifanya,
Hakuna tena namna, wala usije danganya,
Na usiseme hapana, kwamba wewe hajafanya,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.

Hatufuti kwa kubisha, Kumbe kosa umetenda,
Utakuwa wajichosha, Wajiwekea kidonda,
Moyo wajihuzunisha, Wajua ulivyotenda,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Huna furaha moyoni, makosa ndio sababu,
Kosa hutafuna ndani, ukikataa kutubu,
Huiondoa amani, dhamiri yakusulubu,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Unapotubu tambua, usilete mazoea,
Nikikosa namwambia, Mi mwanadamu ajua,
Hayo makosa jutia, amua hutarudia,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.

We si wakwanza kukosa, kwamba watu watacheka,
Nisamehe nimekosa, waungwana hutamka,
Ujifunze kwao sasa, kwenye kosa utatoka,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Msamaha una nguvu, kuyaponya majeraha,
Unakupa utulivu, pia moyo wa furaha,
Watu wale wapumbavu, hukimbia msamaha,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Ukiombwa usamehe, sio hadi usifiwe,
Msamaha Si sherehe, na zawadi uletewe,
Kazi yako ni samehe, na kinyongo uondowe,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea. Kweli amekukosea, Sikatai natambua,
Unapo mfikiria, hasira kumjengea,
Maumivu wapalia, bora tu kumuachia,
Kwa kupenda kusamehe, Maumivu unafuta.
Kovu laweza bakia, lisije kushikiria,
Ushindwe kumuachia, samehe na achilia,
Wewe unayopitia, wengine washapitia,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea.
Siwezi kulazimisha, hatua wewe chukua,
Mimi nimeelimisha, ni wewe wakuamua,
Jambo lako linatisha, ila ni ishatokea,
Kuacha au kufuta, wewe ndie changanua.
#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya +255 717 567 500
somavitabuleo@gmail.com

FUTA

Baada ya kuliona, kosa ulilolifanya,
Hakuna tena namna, wala usije danganya,
Na usiseme hapana, kwamba wewe hajafanya,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.

Hatufuti kwa kubisha, Kumbe kosa umetenda,
Utakuwa wajichosha, Wajiwekea kidonda,
Moyo wajihuzunisha, Wajua ulivyotenda,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Huna furaha moyoni, makosa ndio sababu,
Kosa hutafuna ndani, ukikataa kutubu,
Huiondoa amani, dhamiri yakusulubu,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Unapotubu tambua, usilete mazoea,
Nikikosa namwambia, Mi mwanadamu ajua,
Hayo makosa jutia, amua hutarudia,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.

We si wakwanza kukosa, kwamba watu watacheka,
Nisamehe nimekosa, waungwana hutamka,
Ujifunze kwao sasa, kwenye kosa utatoka,
Kwa kulikubali kosa, Njia ya kosa kufuta.
Msamaha una nguvu, kuyaponya majeraha,
Unakupa utulivu, pia moyo wa furaha,
Watu wale wapumbavu, hukimbia msamaha,
Kwa kuomba msamaha, Njia ya kosa kufuta.
Ukiombwa usamehe, sio hadi usifiwe,
Msamaha Si sherehe, na zawadi uletewe,
Kazi yako ni samehe, na kinyongo uondowe,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea. Kweli amekukosea, Sikatai natambua,
Unapo mfikiria, hasira kumjengea,
Maumivu wapalia, bora tu kumuachia,
Kwa kupenda kusamehe, Maumivu unafuta.
Kovu laweza bakia, lisije kushikiria,
Ushindwe kumuachia, samehe na achilia,
Wewe unayopitia, wengine washapitia,
Kwa kupenda kusamehe, furaha wajiletea.
Siwezi kulazimisha, hatua wewe chukua,
Mimi nimeelimisha, ni wewe wakuamua,
Jambo lako linatisha, ila ni ishatokea,
Kuacha au kufuta, wewe ndie changanua.
#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya +255 717 567 500
somavitabuleo@gmail.com

Powerful πŸ’ͺπŸ’ͺ@Regrann from @mwlmakwaya - KONDAKTA NA ABIRIA

Abiria : Hivi nyie makodakta mtaanza lini ustaarabu 'aliongea kwa ukali'

Kondakta : Tumeanza leo na sasa hivi.

Abiria : Mbona nimekuomba msaada unishushe hapo umegoma?

Kondakta : Konda mstaarabu humshusha abiria kwenye kituo halisi kinachotambulika.
Abiria : Mbona mnapakia popote pale kwenye kushusha ndio mnaleta ujuaji.

Kondakta : Unaweza pokea pesa kwa mtu yeyote lakini hupaswi kutoa pesa kwa yeyote. Maana unapopokea unaweza amua kuzirudisha kwa kuwa zipo mikononi mwako ila ukitoa unaweza usirudishiwe. Na huo ni ustaarabu unaweza jifunza kwetu makonda.

Abiria : Kwa hiyo unajitia mjuaji?

Kondakta : Kwasababu wewe hujui lolote ndio maana unataka kama ulivyopanda popote ndivyo ushushwe popote.
Abiria : Si nimekuomba lakini.

Kondakta : Ndio maana mnaonaga Mungu hawajibu mkimuomba. Mungu anakujibu ukiwa kwenye kituo, ila anakuchukua ukiwa Katika hali yeyote mbaya hana hiana anakuchukua harafu anakufundisha utaratibu.

Abiria : Kwa hiyo unamuingiza Mungu kwenye uonevu wako. Unadhani anakusikiliza

Kondakta : Basi muingize wewe kwenye uonevu ulioonewa.
Dereva : Kwani tatizo nini 'dereva aliingilia huku akicheka'

Abiria : alichonifanyia konda wako unadhani ni kitu kizuri.

Kondakta : Sio huyo mwalimu wa ustaarabu wakati yeye mwenyewe sio mstaarabu. Amekaa siti ya mbele baada ya kukuomba wewe dereva umshushe anahangaika na konda sio mstaarabu.

Dereva : Mimi nimemnyamazia anaongea ustaarabu wakati amepanda kwenye gari tuko wawili tu huku hata salamu hajatoa. Halafu... Abiria wengine : Kicheko hahahahaha
Kondakta : Haya mstaarabu shuka hiki ndio kituo
Abiria : Tutakutana tu jifanye mjanja.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya. - #regrann

BINTI NA MAMA YAKE
Binti : Hivi mama, kwanini uliamua kuolewa na baba?

Mama : Upendo wake ulinivutia sana.

Binti : Upendo tu, hamna kingine kilichokuvutia?

Mama : Hahaha mwanangu, unajua Upendo hufanya uone kila kitu tofauti na wengine waonavyo.
Binti : Kwani wanaume wengine hawakuwahi kukupenda?

Mama : mmmh walikuwepo na walinipenda tena inawezekana walinipenda kuliko hata alivyonipenda baba yako. Ila Upendo wao haukuongea lugha ninayoielewa.

Binti : Upendo na lugha tena Mbona unanichanganya.

Mama: Kuwa na uwezo wa kuongea hakumaanishi ndio Kuwa na uwezo wa kueleweka. Hivyo kujua kupenda haimaanishi ndio kujua kuonesha huo Upendo kwa unayempenda.

Binti : Kwa hiyo hamjawahi kugombana au kutofautiana hadi ukatamani usingeolewa naye?

Mama : Kwa kweli imeshatokea. Lakini mimi na baba yako ni marafiki na si unajua marafiki kama hamjawahi tofautiana ujue mmoja wenu au wote ni wanafiki.
Binti : Kwani na ninyi mlikuwa mnakula bata enzi zenu.
Mama : hahahaha kila enzi ina enzi. Kila mziki una aina yake ya kucheza. Tofauti yetu na ninyi ni kwamba bata mnaweka mbele kabla ya kutengeneza banda. Yaani namaanisha starehe ni baada ya kazi. Hata Mungu alistarehe baada ya kazi ila ninyi kazi hamtaki mnataka starehe ndio maana hata wanaume mnataka waliokwisha fanikiwa Kuwa na mali na sio wanaowapenda hata kama wanavitu kidogo.

Binti : Mmh mama ndio unatunanga
Mama : Kwani uongo si ulilalamika wewe wakati nimemwachisha dada wa kazi. Unadhani ungekuwa unajua kupika kama sio kukusimamia kidete. Kupika kufua kuosha vyombo hamjui ila kila kumbi za starehe mnazijua. Halafu mnataka muwe na ndoa nzuri.
Binti : Eeh mama basi, Kwani mi nilikuuliza hayo.

Mama : Umenianza mwenyewe sasa tulia hivyo hivyo unisikilize. Kipindi chetu sio kwamba tulikuwa hatutongozwi ila kujiheshimu na kujitunza kulitusaidia sana. Sasa nyie leo ukifuatwa na mkaka yaani kila msichana atajua umefuatwa, unadhani kwa kijana anayejiheshimu akisikia hiyo tabia yako hata kama anakupenda hakufuati ng'oo. Mtaendelea kufuatwa na wanaotaka kuwachezea maana hao hata wakisikia umewasema vibaya wala haiwasumbui watakung'ang'ania mpaka unadhani anakupenda unamkubalia. Kwa Kuwa amekufuatilia muda mrefu..

MWALIMU NA MWANAFUNZI

Mwl : Kwanini umefeli hivi?

Mwn : Kwanini na wewe umefeli hivi?

Mwl : Nani amefeli kati yangu mimi na wewe?

Mwn : Wote mimi na wewe tumefeli. Mimi nimefeli kukariri na wewe umefeli kunikaririsha.

Mwl : 'Mwalimu kwa ukali' mjinga wewe nani anakukaririsha. Natoa muda wangu kufundisha halafu unasema nakukaririsha.

Mwn : Katika kufundisha kuna kuelewesha na kukaririsha. Sasa wewe kuelewesha hujui ila kukaririsha unajua cha ajabu umeshindwa kunikaririsha hadi nimefeli.

Mwl : Kwa hiyo mzazi wako alivyokuleta na kuniomba nikusaidie ufaulu masomo ya sayansi alikuwa hana akili.
Mwn : Sio kwamba hana akili anazo sana hata wewe unazo sana. Tatizo mliniona sina akili nilipowaomba nguvu mnayotaka kutumia kunifundisha sayansi mtumie kunifundisha masomo ya sanaa. Wewe na mzazi wote mlinikata jicho na kuniambia ninyamaze sijui dunia inataka nini?
Mwl : Kwa hiyo ushajua dunia inataka nini?
Mwn : Ndio mimi najua, kabla hata hujafeli kunikaririsha nilishawaambia dunia inataka nini kutoka kwangu.

Mwl : Pumbavu!mjinga sana, Kuwa na adabu hujui unaongea na mwalimu.

Mwn : Nisamehe mwalimu nafikiri umesahau Kuwa unaongea na mpumbavu na mjinga asiyependa kukariri kabla hajaelewa.

Mwl : Hivi hujui huna maamuzi hadi ufikishe miaka 18. Sasa hivi wewe ni mtoto unatakiwa kufuata kila kitu unachoambiwa na wazazi na walimu wako alaaah.

Mwn : Nimeelewa sasa.

Mwl : Umeelewa nini?
Mwn : Kwanini watu wengi wakivuka miaka 18 ndio ujinga wao huonekana vizuri. Maana kipindi cha kuuondoa ujinga walifumbwa midomo na hawakuruhusiwa kuuliza zaidi ya kufanya tu.

Mwl : Kuwa makini na maneno yako, kwa hiyo hapa mimi ni mjinga.

Mwn : Hapana sijasema ila kumbuka Mimi sijafikisha miaka 18.

Mwl : Embu nenda dukani kaniletee Kalamu ya kusahihishia mitiani yenu

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

MTU MMOJA ALINIULIZA

swali: Kwanini hufanikiwi kama fulani.
Jibu: Kwasababu Mimi sio kama huyo fulani, sifanani naye hata sura.
Swali: Sikumaanisha hivyo. Nimemaanisha huoni yeye ana viwanja, ana nyumba ana pesa nyingi na anafundisha kama wewe. Kwanini wewe huna?

Jibu: Mimi nimemaanisha hivyo. Kwamba mimi siyo yeye ndio maana sasa sina viwanja nyumba na vyote ulivyotaja, mimi sifundishi kama yeye wala yeye hafundishi kama mimi ingawa wote tunafundisha, ila Mimi sio yeye na yeye sio mimi.
Swali : Kwanini hufanikiwi kama wewe.

Jibu : Nikatabasamu kabla ya kujibu. Hilo ndio swali la msingi. Ki Ukweli tofauti yangu na yule ni kwamba labda yeye amejitafuta na amejipata mapema. Mimi nilikuwa bado namtafuta huyo wewe unayemuona ndani yangu. Ili nifanikiwe kama mimi (mimi ndani yangu)

Swali : Kwani kuwa na mashamba mali na pesa kama yule ni vibaya?

Jibu : Sio vibaya hata kidogo ila kuishi kama yule na kusahau kuishi kama wewe itakupelekea Kuwa mtumwa. Na moja ya kitu kinaweza kuwa chambo cha kutamani kuishi kama yule ni kuangalia na kuvutiwa sana na vitu vinavyoonekana.

Muulizaji : Aaah nimeelewa sasa. Huna shida na Kuwa na mali ila unashida na kuwa wewe kabla ya kuwa na mali.

Mimi : Naam umeelewa vyema sasa katoe sadaka ya shukurani.

Kumbuka:
Ni vizuri kujifunza kwa watu kuliko kujilinganisha ambako kutaleta mashindano.
Mtafute yule wewe aliyendani yako. Wewe ambaye ameumbwa afanye vitu tofauti na yule. Kisha fanya ufanyalo uhakikishe huyo wewe anafanikiwa kuishi kile alichokuja kuishi ndani yako maana muda wake ukiisha wewe huondoka akiwa na maana tofauti ya mafanikio na yule.

Swali : Kwanini hufanikiwi kama wewe?

Onyo:
Mafanikio yasiyohusisha mambo ya kiroho, kihisia, kijamii bado hayajakamilika hata kama tutayaita mafanikio dunia nzima.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

KUTOA KUBAKIZA MOJA

Unapofanya maamuzi unakuwa na chaguzi nyingi. Unazipunguza zinabaki chache, na katika chache kuna moja linakuvutia na linaonekana na nguvu kwako na unaamua kulichukua kwa kuamua. Unakuwa umetoa yote na umebakiwa na moja.

Ulipohamia huo mji ulikuta makanisa mengi sana. Na yote ni mazuri, lakini katika yote ukaamua kuchagua moja na kuwa kanisa lako unalotambulika Kuwa u mshirika. Hapo napo umetoa mengi umebakia na moja.

Kabla hujaoa/hujaolewa ulifuatwa au uliona wengi sana. Wazuri wa kila rangi, wenye maumbo na mwonekano wa kila namna. Lakini uliamua kuwatoa wote na kubakia na mmoja. Hiyo pia ni kutoa kubaki na moja.

Kuna Mungu na Ibilisi, kwenda nao wote haiwezekani inabidi tu utoe ubaki na mmoja. Hiyo nayo ni kutoa na kubaki na moja.

Nimekuja kugundua katika maisha watu wanapenda kubaki na vingi. Yaani watoe vichache wabaki na vingi. Sasa katika mambo muhimu karibia yote unalazimika kubaki na moja. Sasa wengi hatupendi ndio maana
-Tuna watu wasio na msimamo wao ni ndumilakuwili mtu wa nia mbili.
-Tuna watu hawajulikani wanaabudu wapi. Wao ni kama watalii kila mbuga twende tu.
-Tuna watu hawana maono wao kila njia twende. Kila mtu maarufu au aliyefanikiwa anataka kuongozana naye.
-Tuna watu wao hawataki kuoa sio kwamba hawezi kupata mwanamke mmoja hapana ila anataka abaki hivyo ili kila anayemtaka awe naye.

Hayo na mengine mengi yanahitaji mtu anayeamua kutoa na kubaki na moja.
Uzuri ni kwamba ukifanya maamuzi mazuri ya katika mambo ya kubaki na moja. Basi hiyo moja itakusaidia kukupa vitu ambavyo ulivyoondoa visingeweza kukupa. Chagua kubaki na moja ambayo ndani yake hiyo moja kuna vingi furaha na amani na utajiri vikiwemo kati ya vingi vinavyopatikana ndani ya hiyo moja.

Ufunguo.
KUTOA=KUONDOA.

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Unapoongea vitu vigumu kwa lugha nyepesi haifanyi vitu hivyo Kuwa vyepesi bali unawafanya wanaokusikiliza kuamini uwezo wao ni mkubwa kuliko vitu hivyo na hiyo ndio maana ya kuhamasisha." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Kuhangaika kutamani umbo la mwingine ni sawasawa na kuhangaika kukariri namba ya simu ya mtu mwingine ili hali ya kwako huijui, hakukufanyi namba yake Kuwa yako"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Nimesikia watu wanapenda kusema 'nakupenda bure' au 'Nisamehe bure'. Hivi hamjui kupenda ni gharama; vipi kwenu kuna watu wanasamehe kwa pesa?" #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Mungu asiye na mipaka amejiwekea mipaka, wewe uliye na mipaka unataka uhuru wa kufanya kila kitu. Acha ujinga jiwekee mipaka hata kama unapenda kuvuka na unaona haina shida hata ukiivuka, tafadhari usiivuke." #Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

"Unapokuwa kijana hizi hatua 4 ni za muhimu sana sana, sababu chaguzi hupungua kwa kadri umri unavyosonga CHAGUZI ⬇ TAFAKARI ⬇ MAAMUZI ⬇ MATOKEO

Matokeo yeyote ni matokeo ya chaguzi tulizofanyia maamuzi iwe kwa kutafakari au kutokutafakari"

#Fikicha Akili#

JIFUNZE KUJIFUNZA
Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.

Most Popular Instagram Hashtags