swahilitimes swahilitimes

14,874 posts   284,671 followers   0 followings

Swahili Times  Habari na burudani bila mipaka - saa 24.

Mamlaka ya Wanyamapori nchini #Kenya (KWS) imetahadharisha kuwa Simba nchini humo watatoweka ndani ya miaka 15 hadi 20 kama jitihada za kuwalinda hazitafanyika. Kwa sasa Kenya ina Simba chini ya 2,000, na hupoteza Simba 100 kila mwaka kutokana na ukame, ongezeko la watu, rushwa.

Mamlaka nchini #Zambia imepiga marufuku kinywaji cha kuongeza nguvu (Natural Power SX) baada ya kubainika kuwa na viambata vya Viagra. Mtuamiaji kutoka #Uganda alidai uume wake ulisimama kwa muda mrefu baada ya kukitumia.

Licha ya kinywaji hicho kuzuiwa, bado kinaendelea kuuzwa kwenye maduka mbalimbali jijini Lusaka.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kujenga mazingira ya uwekezaji, kupambana na rushwa na ujenzi wa miundombinu. Wawili hao walizungumza kwa simu jana, na kuridhia kuendelea kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo.

#Instagram imetangaza kuwa inaleta huduma (checkout) itakayowawezesha wanatumiaji kununua bidhaa kutoka kwa wauzaji kwa kutumia mtandao huo kufanya malipo, na kuweka anwani zao ili kufikishiwa bidhaa zao. Wauzaji watatakiwa kulipa ada, ambayo kiwango chake bado hakijawekwa wazi.

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, ameijia juu mikoa iliyoshindwa kufikia lengo la ujenzi wa viwanda 100 kwa mwaka kwa kila mkoa, na hivyo ameagiza ifikapo Juni mwaka huu mikoa hiyo iwe imefikia lengo, sivyo, ataitaja hadharani.

Jafo ameyasema hayo wakati akipokea ripoti ya ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa kwa kipindi kinachoishia Disemba 2018.

Waziri huyo ameeleza kuwa, hadi Disemba 31, 2018 jumla ya viwanda 4,777 sawa na asilimia 183.73 vilikuwa vimejengwa, ambapo lengo lilikuwa ni kujenga viwanda 2,600.

Kurasa za magazeti ya Tanzania leo Alhamisi Machi 21, 2019..

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji (PIC) imeishauri serikali kuchukua jukumu la kulipa deni lenye thamani ya TZS trilioni 1.39 ambalo TANESCO inadaiwa na IPTL, PAET, TPDC na benki, kutokana na shirika hilo kuelemewa na madeni, lakini pia deni hilo kuendelea kuongezeka kutokana na riba.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imezuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki hadi kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi ya kuomba
kutengua uamuzi wa Spika wa kumfuta ubunge Joshua Nassari itakaposikilizwa na uamuzi utolewe.

Mchezo wa kwanza robo fainali ya Mabingwa wa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe utachezwa Dar es Salaam Aprili 6, 2019. Timu hizo zitarudiana tena baada ya wiki moja nchini DR Congo, na mshindi katika michezo hiyo miwili atafuzu hatua ya nusu fainali. #CAFCLDraw

Matokeo ya droo ya Mabingwa wa Afrika: #CAFCLDraw

Simba SC vs TP Mazembe
Mamelodi Sundowns vs Al Ahly SC
Horoya FC vs Wydad Casablanca
SC Constantino vs Esperance Sportive

Matokeo ya droo ya fainali za Kombe la Shirikisho la CAF, iliyochezeshwa leo. #CAFCLDraw

Tanzania imeshika nafasi ya 153 katika orodha ya nchi 156 zenye furaha zaidi. Uorodheshaji wa nchi hizo umezingatia uwezo wa kiuchumi, umri wa kuishi, huduma za kijamii na uhuru wa kufanya machaguzi katika maisha. Finland inaongoza duniani, huku Sudan Kusini ikiwa ya mwisho.

Most Popular Instagram Hashtags