raymsoma raymsoma

137 posts   2,972 followers   690 followings

Raymond Msoma  My Offial Instagram Page 📖 Education: BAF 🦂Team: Scorpions 🎂Birthday: November - 11 📬Address: P.o.Box 743 Dsm 📧Email: mmasi2005@hotmail.com

Eid Mubarak

#Eidmosifresh Hii sio ya kukosa ni Siku ya Eid Mosi ndani ya Junction Pub Changanyikeni, Chuo Kikuu Mlimani (UDSM), Burudani zakutosha kutoka kwa DJs @timesfmtz @djd_slash @deejay_ninaa @djpoison255 wakishirikiana na wasanii wa bongo flava wakiwemo @linexsundaymjeda @mycoely @mabantuofficial @belleyoung_tz @brianlorenzotz

Zinidine Zidane anakuwa kocha wa kwanza kubeba UCL mara 3 mfululizo, mabao mawili aliyofunga Gareth Bale yanamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mara mbili akitokea sub katika Fainali ya UCL.

Real Madrid wanakuwa timu ya kwanza kubeba UCL mara tatu mfululizo, na kwa timu za Uingereza hii inakuwa fainali ya 7 kupoteza dhidi ya timu kutoka Hispania.

Hii ilikuwa fainali ya 16 kwa Real Madrid, ukiondoa mwaka 1962 walipofungwa na Benfica, mwaka 1964 walipofungwa na Inter Milan na mwaka 1981 walipofungwa na Liverpool. Fainali 13 zilizobakia Madrid wamefanikiwa kupata ushindi.

MSIMU WA 2004-2005.

1.Liverpool ilimfunga Fc Porto kwenye Uefa.

2.Wakati Michael Owen aliyekuwa akivaa jezi namba 10 kulazimisha kwenda Real Madrid.

3.Liverpool ilifungwa mabao 2-1 na Manchester United Old Trafford, Sylvester akifunga bao 2 huku O'shea akijifunga.

4.Liverpool iliitoa klabu ya Uingereza kwenye Uefa ambayo ni Chelsea.

5.Liverpool ilikuwa na mchezaji kutoka Senegal ambaye ni Salif Diao.

6.Liverpool ikabeba taji la UEFA msimu huo.

MSIMU HUU WA 2017-2018.

1.Liverpool imeifunga Fc Porto kwenye Uefa.

2.wakati Philippe Coutinho aliyekuwa anavaa jezi namba 10 kulazimisha kwenda Barcelona.

3.Liverpool imefungwa mabao 2-1 na Manchester United Old Trafford, Rashford akifunga bao 2 huku Bailly akijifunga.

4.Liverpool imeitoa klabu kutoka Uingereza kwenye Uefa ambayo ni Manchester City.

5.Liverpool ina mchezaji kutoka Senegal ambaye ni Sadio Mane.

6.Je, Liverpool itaweza kubeba Champions League kutokana na tukio la mwaka 2005?

Ushindi Waliyoupata Brighton Wa Goli 1-0 Dhidi ya Manchester United Umekuwa Ni Ushindi Wao Wa Pili Tangu Walipofanya Hivyo Novemba 6, 1982.

#TBT, I appreciate how much you have done for me. May God bless you have a great Day. Happy Women's Day #08/03 #raylibrary

Napenda kuchukua Nafasi Hii Kutoa shukrani zangu za Dhati kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki ambao kwa namna moja au nyingine waliwezesha mafanikio yangu kwa mwaka 2017 pasipo nyinyi nisingekuwa hapa nilipofikia baadhi ya ndoto zangu naomba muendelee kuwa bega kwa bega niendelee kutimiza ndoto zangu.
Naimani palipo na mafanikio vikwazo havikosekani hivyo basi kama nilikukwaza kwa namna moja au nyingine naomba tusameheane maana hakuna aliyekamilika kila mmoja wetu ana mapungufu yake.

Ningumu kukumbuka wote naomba Umtag mtu yoyote unayehisi anamchango mkubwa kwangu na kwako pia ili tuukaribishe vyema mwaka mpya 2018 na uwe wa mafanikio zaidi kwetu sote.

1.Safari Suit By @speshoz
2.Photo By @chrisdcreativevisuals

#TBT 2007 Afro Man with Nokia Tochi @dodoma_tz

Mapema #25/11/2017 Ofisini kwa Kamanda wa Jeshi la Police Mkoa wa Mbeya RPC Mohamed Mpinga nikiwa na wanajopo wenzangu toka @timesfmtz

Vibe La #NewacityPub #TimesFMTZ Wanafanya #MapinduziYaBurudani. Kama Una Muda Na Upo Maeneo Ya Karibu Jisogeze Tujiachie Pamoja. 95.3 #TimeFM Mbeya #MgusoWaJamii @sandytemu @hellenmnzava @idriskitaa @lilOmmy @raymsoma @alen_donald @didahshaibu @goyayiz @didahshaibu

#Niponye ni wimbo ambao @abeid_tz aliuandika alipopata matatizo ya ulemavu kama alama ya kuonesha kumwamini Mungu kuwa anaweza kufanya yote.

HISTORIA YAKE ILIKUWA HIVI:

Jina langu ni Abeid Makarabo , ninamiaka 26 tangu Bwana alipo nileta duniani kupitia kwa Wazazi wangu Rhonda Mgombozi na Madaraka Makarabo huko Kaliua mkoani Tabora.

Nilipata elimu ya msingi mwaka 2000-2006 pale Kaliua shule ya msingi . Mwaka 2007 nilianza masomo ya upili kupitia shule ya sekondari ya mtakatifu Vicennt wa Paulo iliyoko Urambo mkoani Tabora ambako nilisoma mpaka kidato cha pili .

Mwaka 2009 nilihamia shule ya sekondari ya Minja iliyoko Masumbeni-Ugweno mkoani Kilimanjaro ambako nilihitimu kidato cha nne. Huku ndiko nilimpokea Yesu na kupata ubatizo kupitia kanisa la T.A.G Masumbeni na ndiko karama yangu ya uimbaji ilipo chanua zaidi kupitia vipindi vya sifa na kuabudu kupitia CASFETA

Mwaka 2011 nilifanikiwa kujiunga kidato cha tano katika shule ya sekondari Karatu. Baadae nilihamia Kaliua sekondari ambako nilisoma na kuhitimu kidato cha Sita
Baada ya kukosa sofa za kusoma shahada ya Udaktari chuo kikuu , ilinilazimu niombe kusoma ngazi ya stashahada ya Utabibu ambayo kwa mwaka huo sikuipata nafasi.

Baada ya kukosa nafasi ya kuendelea na masomo kwa mwaka wa masomo 2013-2014 , niliweka matumaini kwa mwaka wa masomo 2014-2015.

Nikiwa nasubiri muda huo ufike sikutaka kubweteka. Ikanibidi nijihusishe na maswala ya kufundisha masomo ya ziada (tuitions ) kwenye vituo kashaa ikiwemo kile cha The Ambitious education centre cha Tegeta , pamoja na Mesak Mwenge. Pamoja na hayo pia nilijishughulisha na kazi za mapokezi katika hotel ya Kebby's iliyoko Bamaga -Dsm.
Baadae niliona maslahi ya kufundisha hayakidhi mahitaji yangu . Niliacha na nikajiunga na kampuni ya ulinzi OGM iliyo kuwa na dhamana ya usalama wa jengo la Viva Tower lililiko Posta-Dsm . Huko nilikua na majukumu ya kusimamia maegesho ya magari yaliyo gorofani , pamoja na kusimamia camera za ulinzi CCTC .

Kwa kiasi kazi hii ilikuwa na maslahi ingawa 22 June 2014 nililazimika kuacha kazi kwasababu hali ya afya yangu ilianza kuzorota .Nilitafuta matibabu ktk hospital kadhaa hapa Dar kama vile Lugalo , Muhimbili na Aga Kh

Most Popular Instagram Hashtags