official_16_april official_16_april

46 posts   24,162 followers   99 followings

APRIL  πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Part 2
.
Lakini Babu, ni wewe uliekula chumvi kunizidi maswali mengine sina majibu yake, na sie wewe ulieniambia ya Ngoswe nimuachie Ngoswe? Mbona unataka kuniponza Babu??niliongea kwa kulalamika kweli, "Ebu weka eria vizuri iyo tuendelee kusikiliza yaliyojiri" alisema babu kanakwamba hakusikia malalamishi yangu,
'
"Babu betri zimekwsha hizi, redio imezima, Nikimbie dukani Mara moja kuleta betri mpya" nilisema
'
"Zima moto huo twende tukalale, Giza limeingia hakuna haja ya kupoteza muda kwenda dukani wakati hata tukiwasha redio kesho bado itaongea tu,
'
"Lakini tutakuwa tumepitwa na matangazo ya muhimu ya Leo na si ajabu tusiyapate tena" nilijibu kwa kushangaa
'
"Kama waliokwenda ziwani wamekwisha lala, wewe unahitaji kukaa macho Kama nani??, kwani hao hawajui wakija kesho watakuta matangazo yameshapita"? Sikumuelewa babu kabisa.. Lakini kwakua yeye ndie Alikua mkuu wa Boma, nilikubali amri yake japo kishingo upande nikaenda kulala..
'
Palipokucha nilikwenda kununua betri kuwasha radio nikakuta yameshanipita mengi sana, hadi sasa palikua habari mpya nyingi ..
'
"heh babu eti fundi hamisi mziba makarai amekutwa hai ziwani"? Ivi tungepata zile taa na wale vijana wanamaji si tungemkuta padri Erasimus na yule mama mchoma vitumbua wakiwa hai eeh?"
'
"Kupinda kwa kijiti hakuzuii kuchora mstari ulionyooka" alinijibu babu nisielewe anacho maanisha,
'
"Jiandae uwende na wenzako kuvua upande wa kusini"
'
Lakini babu kuna ajali ziwani.. Meli imezama, '
"Meli imezamia kaskazini, Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi" nilipata jibu jipya tena kutoka kwa babu..
'
Babu unajua sikuelewi kabisa?? Niliuliza kwa hasira.
'
"Asiejua maana haambiwi maana" had wakati huo nilishamchoka babu, nilijiandaa nikabeba ndoano na nyavu zangu nikaelekea kuvua!
'
Babu akasema "
"

Mkimuona sultani mpeni pole sana kwa kupoteza nguvu kazi, na yule alietuambia tusubiri pakuche, muambie tunaomba atusaidie taa zaidi na zile boti chakavu zitengenezwe kwa hisani yao,.. Pia wasisahau kuwapa makoti ya baridi wale vijana wanamaji, yaonekana wanaogopa baridi sana.. '
Zile familia zilizopoteza watu, Waambieni wakati ujao hatutarudi kulala hadi asubuhi..
:
:KWELI BADO SIJAMUELEWA BABU..
:
:MWISHO.

Ilikua Jioni, Jioni iliyokosa utulivu nimeketi na Babu, sote tukitazama chini kwa tahamaki, mikono yetu yenye nguvu tofauti tofauti ikitetemeka hata kufanya ufanisi wa kukamata kikombe uanze kupotea kabisa..
Babu alitenga kikombe chini akanitazama tena akaniuliza "kwa hivyo mama sharuna amezama"? Rafiki yangu Mzee tambitambi naye hajaonekana hadi muda huu? Nachelea kumuulizia Mtoto wa peter muuza supu, aliniaga hapa akienda kuhemea.
"Babu ni Mara ya tatu sasa waniuliza swali moja, unahisi naweza kutoa majibu tofauti na hayo?? Nilijibu kwa gadhabu kidogo.
:
:
Kila Mara nilisimama kwenye kichuguu kando ya choo chetu kuu kuu nikitegesha mawimbi ya radio yangu ndogo kusikiliza kinachoendelea katika ajali ile ilogharimu Maisha watu pale kijijini kwetu, kila nyumba ilikua na kilio, palikua na msiba, :
:
"Mkuu wa *** ametangaza kusitisha zoezi la uokoaji hadi kesho kutokana na Giza"
Ilisikika sehemu ya taarifa ile ya habari, niligeuka kwa kasi ya mwewe kumtazama babu aliedondosha kikombe na kusimama kwa miguu miwili akitetemeka mabega na meno yakigongana mithili ya mtu aliekua na baridi Kali, : "Giza?? Hivi kumbe kijiji chetu kidogo eeh?? Kweli tumekosa namna nyingine ya kuokoa zile roho za kina mama watoto na wazee?? Wale vijana na kina Baba? Ina maana zile meli zinazotembea usiku huwa zinapapasa?? Mbona kuna zile taa tunazotumia kuvulia senene??mbona naona vijana siku hizi wakimulika sana usiku wakitengeneza tamthilia zao na muziki?? Ivii.. Kipindi kile tunamtafutia Sultani mke? Hatukuwa tunazunguka hadi usiku wa manane tukimulika kila mahali hadi usiku sana na taa zilikuwepo?? Kwani wale vijana wetu wanamaji wako wapi? Yule kiongozi wa vijana wanamaji wa kijiji hakuwapa mafunzo ya kutosha ya kuzama muda na wakati wowote?? Au hawakua na vifaa toshelezi?? Mbona mwenyekiti mzee Hanifu wa kule kando amesafiri usiku huu huu na amefika salama kabisa? Kwanini tusingetumia taa yake kumulika humu ziwani kuliko kwenda kulala tukisubiri machweo?? Nasikia sauti ya Faridi kwa mbali ikiomba msaada kutoka chini kule, mbona wamerudi sasa badala ya kumfatilia kumuokoa?? Ivi wakija kesho watamkuta kweli hata wa kusimulia yaliyotokea katika usiku ule kwa kiza??" Inaendelea.....

This one is for the love of hip hop.. Today my lovely sis September was born @dread_soul_22_pro huwa nafurahi sana siku Kama hii ikikukutia huko mbali na nyumbani, kila nikiangalia kuku nakuta wako wote na wako salama Basi roho inaridhika mno.. Finally unakaribia kukubali kumaliza kusoma..
Happiest birthday didi.. Happy birthday "September" more everything. May the lord protect ur pure heart!! I love you
Along side na family members
@salaya.mary
@babu54g
@imamatemu
@summy_muuu
@meruna_gapcho
@edwardthegoalgetter
@riz_iky110482
It's our sister's birthday yo!!

πŸ™πŸ™πŸ™β€β€ thank you so much Mr anonymous.. And thanks to other people too..
#0752351406 kupitia from 1000 tu.

Asante sana

Habari!! Naimani kila mmoja akichangia ELFU 1, tutafika lengo sio lazima elfu 1 tu hata Kama UNAYO ZAID unaweza kusaidia hawa Watoto na mwenyez mungu akakubariki, tusikutane kwenye kusoma posts na Ku comments au Ku like tu hata kwenye mambo Kama haya tuoneshe umoja na ushirikiano.. Naimani elfu 1 sio kitu hata Kama unayo elf 10 tu.. utaitumia kwa bundle na pengine isitoshe lakn kuna Watoto wanaihitaji hiyo waweze kuishi.
:
Watu 100 mkijitolea elfu moja moja tu au zaidi kwa hisani yenu mtakua mmesaidia Watoto wengi mno

Tumia namba 0752351406(direct to me) :

Au Kama kuna mwenye msaada wa either Nguo, sabuni au material things (Walioko Dar) pls see my DM nikuelekeze mtu wa kumfikishia.. Zoezi lilianza WhatsApp and I'm glad matokeo yalikua mazuri mno
Anything to #0752351406 kwa atakaetuma msaada wake na atahitaji kuwa acknowledged nitam post hapa hapa..
Pls send me a message ukishatuma. Asanteni sana

Precious in the sight of the LORD is the death of his faithful servants!! :
:

Wapumzike kwa Amani wote waliofariki katika ajali ya MV nyerere, Poleni wote mliopoteza ndugu jamaa na Rafiki.

Indirect Rejection.
Sehemu ya 2
:
:
4. Stay away/Leave..
Just Go.. If it's leaving the workplace, mtaa, au mahali ambapo unamuona sana..Give ur heart time kuzoea yanayokuja, Hakuna kitu kinachouma Kama kushuhudia unavokufa(kihisia)
So Kama hauko tayari kwa yote hayo.. Just leave, don't cause a ruckus, Just take ur lesson and leave! Sometimes it's your own fault.. Unataman hata wangeonesha kukuhitaji just once and ujibadilishe but The chances are over.. So what do you do?? Kama kuumia tayari.. Kulia tayari.. Kukesha usiku mzima unawaza tayari. Kushindwa kula tayari.. What's next?? LEAVE. it hurts.. But, so what?? Who cares?? Do they?? No.. At this time, attention yao iko mbali kabisa na wewe, they might try to fake it. Might try to show u this and that.. But moyoni Tayar wameshafanya maamuzi, either of their future, na wameshakutoa, and put someone else.. So instead of wasting hayo machozi.. Huo muda ungekua umefika nusu ya safari,
"these things hurts bana"
:
:
5. Usioneshe maumivu yako..
Take heart, Vumilia tu, just in time utazoea(it might take so long) but at the end it worth it.. Sasa hata ukionesha unaumia inasaidia nn?? Let's say amefariki mtu,mmezika, but unatumia siku nyingi sana kumlilia na kuonesha unaumia sana.. Insaidia nn?? Anarudi?? The least u can do is locking ur self inside. Cry to the end.. Wipe ur tears, smile to them like you haven't noticed anything..
:
:
6. TALK IT OUT IF POSSIBLE
Hapa Kama unaona kuwa unaweza ukaokoa jahazi.. and they give u some hopes.. Find time and talk it out, Kama unaona kabisa it's all dead.. Na hata uongee had kesho you have missed the train alredy.. Start walking tu.
:
:NB: USIONE NAANDIKA KAMA NI KITU RAHIS.. IT'S NOT BUT SAVE UR SELF.. End...

INDIRECT REJECTION..
:
:
There are times in life when u fall for someone.. Unajikuta unampenda sana mtu lakini mwisho wa siku either kwa mapungufu yako mwenyewe au yake.. Ule upendo unayumba Au unakufa kabisa.. Like hawakutazami Kama walivyokua wanakutazama mwanzo, though hawakuambii kuwa "Bwana nimekuchoka" but matendo yao yanaonesha ivyo! Deep inside you feel for them hadi unahisi bila wao Maisha yako yatabadilika sana.. Au utapata mateso mno, but ndio imeshatokea kwamba unaona kabisa the love has changed.. The feelings on their side are dying it kills you inside na huna cha kufanya! Sometimes hata kuwaambia kuwa bwana 'I can notice kwamba I stand no chance" "I can see kabisa kwamba the way you look at me, your feelings and treatments have changed"

Either ulisababisha kwa kukosea hapa au pale.. Au mapenzi yamekufa tu natural death!!.. What do we do now when it comes to that point..
Everyone has their own ideas and ways of solving these issues..
But I remember watu kadhaa walishaniuliza kuhusu hili in my DM.. Mostly case zinafanana au tofaut kidogo.. But yote kwa yote "Mapenzi yamekufa"
:
:
1. Give them their time:-
If someone is tired, haoneshi kwamba anafurahi kuzungumza na wewe tena.. Au haoneshi Kama ako na mipango hai juu yako, no matter how hard you cry at night.. No matter how much inauma na kukutesa, let them have their time as they wish.. Do not force them to reply your messages on time.. To call you.. To pick ur calls.. To do this and that.. Let them be happy if they think happiness Is found mbali nawewe.. If they have other people walioamua kuwapa attention ambayo u thought u deserved.. Let them give that out!! Kubali tu kuwa hili nimeshalikosa.. Yes it hurts.. Yes it kills.. But moyo wa mtu ukishabalika juu yako, there's nothing u can do!..
:
:
2. Accept the reality
Kubaliana na hali, like this time i have lost(this is very hard.. Very hard), but nothing kills more than living In denial.. Hata mtu alieathirika. Akikataa ile hali ya kuwa me nimeathirika, they tend to perish mapema sana.. So the best u can do is accepting kuwa I'm just here for me, accept that things have changed.. Accept that they don't feel the same anymore.
:
:
Inaendelea nextpost

Wivu, Chuki tu na kutesana..😒
#KablaSalaUkamilisheMama

The silent twins 3.
:
:
Baada ya kuishi kwa hali hiyo kwa kitambo na kuona kuwa Maisha yanakua magumu na hawawezi kuji control, siku moja wakaamua ili waweze kuishi kwa Amani na Furaha lazima mmoja wao Afe "ONE OF US HAS TO DIE" walikubalina kwa pamoja.. Na baada ya majadiliano marefu Jennifer aliamua kufa yeye ili June aishi!! Yani wakaamua kuwa wa kufa ni Jennifer!!
:
:
Ilipofika March 1993 ma dokta wakaamua kuwahamisha kwenda kwenda "Caswel clinic" ili wakapate msaada zaidi, lakini kabla ya kuhamishwa alikuja mwanahabari maarufu kipindi hiko aliyeitwa "Marjorie Wallace" kujaribu kuzungumza nao lakini hawakuongea chochote zaid Jenipher alisikika akisema "Marjorie Marjorie, Inabidi nife" Mr Wallace (Marjorie) alipouliza kwann Jenifer afe, kwa utulivu sana Jenifer alijibu "KWA SABABU TUMEAMUA"
:
:
Walitoka Pale wakawa wanaelekea caswel (clinic) wakat wote Jenifer alikua amelala kwenye miguu ya June macho yakiwa wazi, bila kuzungumza kitu, walipofika clinic walijaribu kumuamsha Jenifer lakini ilionekana ha-respond, ndipo walipoamua kumpima na kukuta alishafariki kitambo sana, kifo kilisemwa kuwa cha ghafla na waliendesha vipimo vyote lakini hawakufanikiwa kukuta sumu wala drugs zozote na kifo chake kikabaki cha kushangaza isieleweke vipi alikubali kufa na akafa bila kutumia njia yoyote ile, June alipoulizwa alidai kutokujua chochote kuhusu kifo hicho
:
:
Siku kadhaa mbele Marjorie Wallace (mwanahabari) Alikwenda kumtembelea June.. June alipomuona Marjorie akasema "NIMEKUA HURU HATIMAYE, NIMEKOMBOLEWA, JENNIFER AMEYATOA MAISHA YAKE ILI MIMI NIISHI"
Kwenye kaburi la Jenifer paliekwa Poem iliyoandikwa na June mwenyewe ilisomeka "WE WERE ONCE TWO/
WE TWO MADE ONE/
THROUGH LIFE BE ONE/
REST IN PEACE/.
Baada ya kifo cha Jenifer June alirud kuwa binadamu wa kawaida kabisa anaongea lugha inayoeleweka na kuishi na watu vizuri, na sasa anaishi huko WEST WALES jiran na wazazi wake Japo mambo mengi sana yamebaki siri anaeijua June ambae haziongelei.
:
Inaaminika Mtu pekee anaejua sababu ya kifo cha Jenifer ni June mwenyewe ambaye hajawahi kusema wala kuongea ni namna Gani Jenifer alifariki..
:
:
MWISHO
Swipe kuona maneno ya mwisho yaliyokutwa katika diary ya Jenifer!!

THE SILENT TWINS Part 2.
:
:
Kupelekwa shule tofauti ndo kukavuruga kila kitu kwani walianza Ku act lunatic kabisa.. Huyu huku asipokula, yule hali, huyu akisemeshwa haongei, hawalali, wanakua Kama ma zombie japo wapo shule tofaut tofaut, had wenzao wakawa wanawaogopa kweli, madkatari wakashauri warudishwe tu wakae pamoja tena ili kuepusha yanayoepukika
:
:
Waliporudishwa pamoja sasa wakawa wanatumia muda mwingi sana kujifungia chumbani peke yao na kuandika hadithi katika mtindo wa "Soap opera" (maigizo ya sauti) wakawa wana record na baadhi kumpa Dada yao Rose Kama zawadi
:
:
Siku moja June aliandika kimemo kikiwa na maneno
Nobody suffers the way i do, not with a sister, with a husband yes, with a wife yes,with a child yes, but this sister of mine, a dark shadow robbing me of sunlight, is my one and only tournament" akimlaumu Dada yake kama source ya mateso yake
:
:
Basi wakaanza kuandika hadithi za kikatili na kihalifu wakiwa ndan peke yao, waliandika story za ubakaji, uuaji wa kikatili, ulawiti, na mambo ya kutisha kwa namna ya kufurahia na sio kukanya!! Ni Kama walivumbua their dark side na wakaifurahia mno..
Baadhi ya hadithi walizoandika ni Kama
-Pepsi-cola addict
-pugilist
-discomania and -Tax driver son
:
:
Baada ya hadithi zao kufail kupata recognition kwenye radio wkat huo wakaamua kugeuka kuwa wahalifu wenyewe, wakaanza kufanya uhalifu mdogo mdogo Kama wizi(petty theft), kukabana wao kwa wao na kuchoma majengo, badae walikamatwa wakashtakiwa kwa kosa la kuchoma majengo, Judge bada ya kupitia details zao akaona wale wanasumbuliwa na "matatizo ya akili" akaamuru wapelekwe kwenye kituo cha kulelea vichaa..
Walikaa humo karibu miaka 14, lakini Maisha yao huo nayo yakawa vituko, siku moja pacha mmoja anakula anashiba mwingine anashinda njaa kabisa, kesho yake alieshinda njaa Jana anakula aliekula anashinda njaa(na chakula kilikuwepo).
Waliwekwa kwenye cell tofauti tofaut huko ndan lakini ukimkuta Jenifer amejibanza ukutani kwenye chumba chake, ukienda kwa June unamkuta nae amekaa vile vile.. Hata masaa bila kusogea..
:
:
Itaendelea...

THE SILENT TWINS
:
:
June na Jennifer walikuwa binti wa wahamiaji wa Caribbean Gloria na Aubrey Gibbons walizaliwa mwaka 1963 mwezi April tarehe 11, Gloria alikuwa mama wa nyumbani na Aubrey alifanya kazi kama fundi kwa Jeshi la Royal Air. Muda mfupi baada ya kuzaliwa kwao huko Barbados, familia yao ilihamia Haverfordwest, Wales..
:
:
Hawa mapacha walikua na tabia Fulani Fulani za ajabu kweli.. Lakini kikubwa walikua hawazungumzi na mtu mwingine yeyote isipokua wao kwa wao na kidooogo Dada yao alieitwa Rose.. Na hata wakizungumza isingekua rahisi kuwaelewa kwani walikua na lugha yao pekee waliyokua wakizungumza(creole).. Hii ikapelekea kupewa jina "THE SILENT TWINS"
Ilikua ngumu kuwatenganisha, kwani kila mara walingozana wao kwa wao wakipiga hatua zinazofanana na hata miondoko ya mwili ikiwa sawa sawa kabisa(ni Kama copy ya kila mmoja wao)..
:
:
Kutokana na kuwa Watoto wa ajabu ajabu wasioeleweka pia kuwa Watoto weusi pekee katika jamii yao walitengwa sana shuleni na kuwa "bullied" hii ikawavuruga kabisa wakawa sasa hawazungumzi na yeyote sio wazazi, walimu wala ndugu na ile lugha yao(Bajan creole ikakua kwa kasi mno kiasi kwamba ukiwasikia wanaongea unaweza kuhisi hawatoki sayari hii..
Walipofika miaka 14 walikua Kama Kichaa kwenye macho ya watu, wazazi na ndugu walitumia namna zote za kitaalamu kuwafanya waongee lugha inaeleweka na wazungumze na watu wengine lakini ikashindikana, wakaamua kuwapeleka shule tofauti tofauti za boarding ili kuwafanya waweze kuzungumza na kuhusiana na watu wengine, wenyewe walihisi wanasaidia lakini hawakujua Hapo ndipo wanaharibu kikao..
:
:
Itaendelea...

Most Popular Instagram Hashtags